Thursday, September 7, 2017

KIONGOZI SALAMA

KIONGOZI SALAMA

"Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa nuru ya uzima". Yohana 8:12.
 
Wote wanaosafiri katika njia ile iendayo mbinguni wanahitaji kuwa na kiongozi salama. Hatupaswi kwenda kwa kufuata hekima ya kibinadamu. Ni haki yetu kuisikiliza sauti yake Kristo ikisema nasi tunaposafiri katika safari ya maisha yetu, na maneno yake daima
ni maneno ya hekima....
Shetani anafanya kazi yake kwa juhudi kubwa sana ili kuzizingira na kuziangamiza roho za wanadamu. Ameshuka chini kwa nguvu nyingi, akijua kwamba anao wakati mchache tu wa kufanya kazi yake. Usalama wetu pekee ni kumfuata Kristo kwa karibu sana,
kutembea katika hekima yake, na kuitenda kweli yake. Hatuwezi kuutambua siku zote kwa upesi utendaji wake Shetani; hatujui ni wapi anapotega mitego yake. Lakini Yesu anazifahamu hila za chini chini za adui huyo, naye anaweza kuilinda miguu yetu ipate
kubaki katika njia zile zilizo salama.... "Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima" (Yohana 14:6) Yesu asema. ----- Letter 204, 1907.
Ingekuwa na faida gani njia ile ya moja kwa moja na ya hakika iendayo kule kwenye utukufu, kama pasingekuwako na nuru yo yote ya ile kweli ambayo ingeiangazia njie ile, ili wasafiri wapate kuitamani? Nuru inayoiangazia njia ile ingekuwa na faida gani kama uzima usingekuwamo ndani ya watu wale wanaosafiri katika njia ile, yaani, katika safari ile ya wasafiri kutoka duniani kwenda mbinguni? Wakiwa na usemi ule wa Kristo,usemao, "Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima," wale wote wanaomwamini Yesu, kiongozi wao, wanaweza kutembea kwa imani kwenda mbinguni, wakiwa na hakikakwamba wamo katika njia ile iliyoelezwa katika neno lake kuwa ndiyo njia. ----- Letter
63, 1893.
Wale waendao kwa utii wataijua kweli ilivyo.... Ili kuijua kweli, yatupasa kuwa tayari kutii. Wale ambao mapenzi yao yako katika mambo ya dunia hii hawako tayari kuiacha mipango yao kwa ajili ya mipango ya Kristo. Wanakwenda gizani, wasijue waendako.
Nuru ya thamani ya ile kweli huangaza ghafula juu ya njia ya kila mmoja anayeitafuta. --
--- MS 31, 1886.

No comments:

Post a Comment