1.0Tunapenda kuwakaribisha wageni wote na waumini wa kanisa hili katika
ibada takatifu Sabato ya leo.
1.2 Leo ni sabato ya kanisa la watoto ambapo ibada itaongozwa na watoto wetu, tuwape ushirikiano.
1.3 Leo pia tutatoa sadaka ya rambirambi kila muumini anapaswa kutoa Tshs. 500/= kwa mwezi na kwa wale wanaopenda kutoa kwa mkupuo ni Tshs 6000/= kwa mwaka
1.4 Tunawahimiza waumini wote kuendelea kutoa sadaka kwa ajili ya efoti ya Majohe.
1.5 Makambi ya mwaka huu yatafanyika mwanzoni mwa mwezi julai, gharama za makambi hayo kwa kila muumini ni Tshs. 6000/= anza kutoa mapema.
1.6 Kambi la PFC na Mabalozi la Konferensi litafanyika tarehe 19-26 June, gharama kwa kila mtoto ni Tshs. 20,000/= yaani kiingilio Tshs. 5000/= Nauli Tshs.10,000/= na Chakula ni Tshs. 5,000/= mwisho wa kutoa kiingilio ni tarehe 28/5/2011.
1.7 Tunawatangazia ndoa kwa mara ya tatu itakayofungwa kanisani Mwenge tarehe 22/5/2011 saa 9 alasiri kati ya Emmanuel Selemani mshiriki wa Mwenge na Saphiness Nicholous mshiriki wa Ilala.
1.8 Kanisa linatangaza nafasi ya kazi ya walinzi wawili wa Kanisa kwa mshiriki yeyote anayehitaji aonane na Katibu wa Kanisa.
1.9 Kesho siku ya jumapili hapa kanisani kutakuwa na semina ya ujasiriamali wote mnakaribishwa kuanzia asubuhi.
1.10 Wale waliotoa ahadi za kuchangia Idara ya Uchapaji kununua vitabu mnakumbushwa kutimiza ahadi zenu.
1.11 Rally ya Konferensi iliyokuwa ifanyike hapa Kanisani kuanzia kesho imehairishwa.
1.12 Mzee wa zamu wiki ijayo ni A. Marwa na Mzee wa zamu Kanisa la watoto L. Mahinyira.
2.0 WAGONJWA:-
vMzee Washington Bomani ni mgonjwa yuko nyumbani kwake.
vMzee Ibrahim Mteleka anaumwa yupo nyumbani kwake
mchikichini.
Tuendelee kuwaombea hao wagonjwa.
Asante!kwani waumini wengine tulio mbali tunapata matangazo.mussa j.
ReplyDelete