Hizo ni baadhi ya picha za waimbaji wa kikundi cha Ambassador of Christ toka Rimera SDA Church nchini Rwanda wakimsifu MUNGU katika uzinduzi wa DVD ya kikundi cha Accacia Singers tarehe 8 mei, 2011 ndani ya viwanja vya PTC jijini Dar es Salaam.
Waimbaji hao wa Ambassodor of Christ toka Rwanda walipata ajali siku ya jumatatu usiku tarehe 9 Mei, 2011 maeneo ya Kahama wakiwa safarini kurudi kwao Rwanda toka Dar es Salaam kwenye uzinduzi . Katika ajali hiyo watu watatu walifariki na wengine watatu wako kwenye hali mbaya.
Hao hapo juu ni miongoni mwa waliofariki, huyo wa juu ni Philbert Manzi na huyo wa chini mwenye chupa ya maji ni Gatare Ephraim. BWANA alitoa BWANA ametwaa jina la BWANA libarikiwe.
Serikali ya Rwanda ilituma helkopta yao haraka kuchukua miili hiyo pamoja na hao majeruhi walio katika hali mbaya.
Mtunzi mmoja wa nyimbo aliandika hivi,
“mara nyingine hatuelewi kwanini shida zinatupata, ........ furahi ndugu mtazame YESU, siku moja tutaelewa”
Mwingine aliandika hivi;
“Baada ya dhiki kuu shida zote zikipita kwenye nchi ile njema tutaimba wimbo mzuri.......... Ndugu jamaa marafiki tutawaona huko juu kwenye nchi ile njema tukiwa na YESU BWANA”
ROHO wa MUNGU aliyemfariji mkuu akafariji ndugu, jamaa na marafiki wote waliofikwa na msiba huo.
Tuombe MUNGU ili tushike maagizo yake ili siku moja tukaimbe wimbo mzuri pamoja na wapendwa wetu hawa.
Tuendelee kuwaombea wapendwa wetu ambao wako katika hali mbaya.






No comments:
Post a Comment