1. Tunapenda kuwakaribisha wageni wote na waumini wa kanisa hili katika
ibada takatifu Sabato ya leo.
2. Baraza la kanisa litakaa tarehe 16/2/2011, wajumbe leteni taarifa zenu mapema.
3. Wale walioahidi kwa ajili ya efoti ya Majohe kumbukeni kutimiza ahadi zenu, efoti inaanza wiki hii, pia tuwaombee wainjilisti wetu watakaokuwa kwenye efoti hiyo.
4. Makambi ya mwaka huu yatafanyika mwanzoni mwa mwezi julai, gharama za makambi hayo kwa kila muumini ni Tshs. 6000/= anza kutoa mapema.
5. Leo na kesho kutakuwa na semina ya uwakili hapa kanisani kwetu itaendeshwa na mkurugenzi toka Konferensi wahusika ni Mzee wa Kanisa, Kiongozi wa Uwakili, wahazini, mashemasi wakuu.
6. Leo tunatoa sadaka kuchangia ujenzi wa kanisa la Chamwino Dodoma.
7. Kanisa linatangaza nafasi ya kazi ya walinzi wawili wa Kanisa kwa mshiriki yeyote anayehitaji aonane na Katibu wa Kanisa.
8. Juma la maombi la afya litaanza tarehe 11/06/2011.
9. Sabato ijayo ni siku ya chama cha mabalozi hapa kanisani.
10. Mzee wa zamu wiki ijayo ni Msafiri John na Mzee wa zamu Kanisa la watoto Maurice Rondo.
No comments:
Post a Comment