1.0 SHULE YA SABATO:
2:00-3:00 Darasa la Waalimu: Idara ya Vijana
3:00-3:15 Nyimbo Shule ya Sabato: Damas Mahimbali
3:15-3:45 Shule ya Sabato: Idara ya Vijana
3:45-4:45 Mwongozo wa kujifunza Biblia: Uongozi wa Shule ya Sabato
2.0 MATANGAZO YA KANISA:
v 4:45-5:00 Matangazo: Mzee wa Kanisa wa zamu
2.1 Tunapenda kuwakaribisha wageni wote na waumini wa kanisa hili katika
ibada takatifu Sabato ya leo.
2.2 Leo tunahitimisha masomo ya wiki ya afya ambayo yamekuwa yakiendelea hapa kanisani kwa wiki nzima.
2.3 Leo ni sabato maalumu ya Idara ya Vijana kanisani, mchana watakuwa na vitu vya kuonyesha, wote tukumbuke kurudi mchana.
2.4 Makambi ya mwaka huu yatafanyika mwanzoni mwa mwezi julai, gharama za makambi hayo kwa kila muumini ni Tshs. 6000/= mwisho wa kutoa fedha ni tarehe 25/6/2011.
2.5 Baada ya ibada viongozi wafuatao wabakie nyuma kuonana na mzee mlezi wa idara hizo, viongozi wote wa kwaya, idara ya vijana, mhazini na mashemasi wakuu wote.
2.6 Vijana wetu wa Mabalozi (Ambassador Club) na Watafuta Njia (PFC) kesho wataondoka kwenda kwenye kambi lao huko Mount Ararat-Mlandizi, tuwakumbuke kwenye maombi.
2.7 Tutakuwa na meza ya BWANA tarehe 2/7/2011 wote tujiandae kushiriki.
2.8 Wajumbe wa kamati za mtaa kwa ajili ya makambi mkutane leo saa 9 alasiri, wajumbe hao ni; Viti na Mahema-Samwel Adam, Chakula-Samwel Jonas, Mawasiliano-E.Marwa, Mimbari-M.Rondo, Ulinzi-Mahimbali,Mapambo-Msafiri John, Afya-Bituro na Mahinyira, Watoto-Naamin Elibahati, Kwaya-Dr. Mchomvu, Mashemasi-Okoth, Shule ya Sabato-Yared Omollo na T. Mbonea.
2.9 Mzee wa zamu wiki ijayo ni T. Mbonea na Mzee wa zamu Kanisa la watoto Mahinyira.
3.0 IBADA KUU:
v 5:00-6:30 WAHUDUMU IBADA KUU:
Mwenyekiti: Idara ya Vijana
Fungu Kuu: Idara ya Vijana
Hubiri: Samwel Adam
Sadaka: Idara ya Vijana
No comments:
Post a Comment