Friday, May 18, 2012

RATIBA YA IBADA: 19 - 05 -2012

SHULE YA SABATO (S.S):
02:00-3:00 Darasa la Waalimu: Uongozi wa Shule ya Sabato
03:00-3:15 Nyimbo za vitabu: Kiongozi wa Nyimbo
03:15-3:45 Shule ya Sabato:Uongozi wa Shule ya Sabato
03:45-4:45 Mwongozo wa Kujifunza Biblia: Wote

MATANGAZO YA KANISA:
04:45-5:00 Matangazo: Mzee wa Kanisa wa Zamu
1.    Tunapenda kuwakaribisha wageni wote na waumini wa kanisa hili katika ibada takatifu Sabato ya leo.
2.    Leo tunatoa sadaka kwa ajili ya kuchangia efoti itakayofanyika Biafra.
3.    Wana wa Kike wabakie nyuma mara baada ya ibada kuna jambo la muhimu.
4.    Sabato ijayo 26/6/2012 itakuwa siku maalumu ya kuchangia ujenzi wa kanisa letu, andaa sadaka yako kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa hekalu la MUNGU.
5.    Zoezi la upigaji picha kwa waumini wa kanisa ili kuweka kumbukumbu katika utaratibu mzuri linaendelea, hakikisha umefikiwa na wahusika.
6.    Tunahimiza waumini kuendelea kutoa sadaka ya gharama ya makambi goli la kanisa letu ni Tshs. 2,021,965/=.
7.    Wazazi na wanachama wa PFC mnaombwa kubaki nyuma mara baada ya ibada, sambamba na hilo kesho PFC & AC watakuwa na mazoezi kuanzia saa 3 asubuhi kwa ajili ya maandalizi ya makambi.
8.    Mahubiri ya Dar es Salaam nzima yataanza tarehe 2/6 hadi 16/6/2012 andaa rafiki wa kuhudhuria nae kwenye mahubiri hayo yatakayofanyika viwanja vya Biafra.

 WAGONJWA/TANZIA:
•    Grace Edward amelazwa Hospitali ya Amana wodi namba 3, tumtembelee na kumuombea.

•    Nelson Luoga amefiwa na mama yake tarehe 17/5/2012 msiba uko kwao Iringa.

IBADA KUU:
05:00-6:30 WAHUDUMU IBADA KUU
    Mwenyekiti:
     Fungu kuu:
    Mhubiri:                   Idara ya Uchapaji 
    Somo la Sadaka:

ANGALIZO: “Uamsho na Matengenezo”

Ellen G. White ana haya ya kusema kuhusiana na ujenzi wa Nyumba ya MUNGU....

“Kanisa linapoanzishwa, kila muumini ainuke na kujenga kanisa. Tunahitaji kuwa na nyumba ya kukutania na ni lazima tuwe nayo. MUNGU anawaita watu wake kuwa wenye furaha na kuunganisha juhudi zao kwenye hilo jambo.

MUNGU anahitaji kujitolea, hii italeta sio u mafanikio ya kiuchumi bali pia mafanikio kiroho. Kujitolea na kujikana nafsi kutafanya maajabu katika maendeleo ya kiroho ya Kanisa”. (Gospel Workers, (House of Worship) uk. 432-433)
ANDAA SADAKA YAKO YA MAJENGO KWA AJILI YA KUFANIKISHA UJENZI WA NYUMBA YA MUNGU.


No comments:

Post a Comment