Friday, May 4, 2012

RATIBA YA IBADA: 05- 05 -2012

SHULE YA SABATO (S.S):
02:00-3:00 Darasa la Waalimu: Uongozi wa Shule ya Sabato
03:00-3:15 Nyimbo za vitabu: Kiongozi wa Nyimbo
03:15-3:45 Shule ya Sabato:Uongozi wa Shule ya Sabato
03:45-4:45 Mwongozo wa Kujifunza Biblia: Wote

MATANGAZO YA KANISA:
04:45-5:00 Matangazo: Mzee wa Kanisa wa Zamu
1.    Tunapenda kuwakaribisha wageni wote na waumini wa kanisa hili katika ibada takatifu Sabato ya leo.
2.    Leo ni siku maalum ya Watafuta Njia na Wavumbuzi, hivyo turudi mchana kujifunza vile walivyoandaa na kuwashauri.
3.    Kesho kutakuwa na baraza la kanisa rasmi, wajumbe zingatieni na mfike kwa wakati.
4.    Tarehe 12/5/2012 yaani sabato ijayo ni mwisho wa kutoa fedha kwa ajili ya mahubiri yatakayofanyika Biafra mwezi wa juni (6), 2012.
5.    Zoezi la upigaji picha kwa waumini wa kanisa ili kuweka kumbukumbu katika utaratibu mzuri linaendelea, hakikisha umefikiwa na wahusika.
6.    Tunahimiza waumini kuanza kutoa sadaka ya gharama ya makambi kuanzia sasa goli la kanisa letu ni Tshs. 2,021,965/= na pia sadaka ya gharama ya efoti ambayo ni Tshs. 5,230,200/= 
7.    Wazazi wa wanachama wa PFC & AC mnaombwa kuwanunulia watoto wenu sare zao mapema.
8.    Tunawakumbusha waumini kutoa sadaka ya rambirambi Tshs. 1,200/= kwa mwezi, tuzingatie hilo.
9.    Wazee wa Kanisa wanaendelea kutembelea waumini.
10.    Mzee wa zamu ni L. Mahinyira.

 IBADA KUU:
05:00-6:30 WAHUDUMU IBADA KUU
    Mwenyekiti: Yohana William
     Fungu kuu: Ezekiel Tumaini
    Mhubiri: A. Marwa
    Somo la Sadaka: Eliamani Sengesa

KWA WATOTO:-
    Yohana William

ANGALIZO: “Uamsho na Matengenezo”

Ellen G. White ana haya ya kusema kuhusiana na Kuharakisha ujio wa KRISTO....

“Kinachotufanya tuendelee kuwa katika dunia hii ya dhambi na huzuni kwa miaka mingi ni kutokuamini, kuipenda dunia, kutokujitakasa na mashindano miongoni mwa wale wanaodai kuwa watoto wa MUNGU.

Tunaweza tukaendelea kubaki katika dunia hii kwa miaka mingi zaidi kwa sababu ya ukaidi, kama ilivyokuwa kwa wana wa Israel, lakini kwa ajili ya KRISTO, watu wake hawapaswi kuongeza dhambi juu ya dhambi kwa kumtuhumu MUNGU juu ya athari za utendaji wao wenyewe usiofaa”. (Maranatha, sura ya 11, uk. 19)

No comments:

Post a Comment