Thursday, April 26, 2012

SABATO YA TAREHE 28/04/2012

SHULE YA SABATO (S.S):
02:00-3:00 Darasa la Waalimu: Uongozi wa Shule ya Sabato
03:00-3:15 Nyimbo za vitabu: Kiongozi wa Nyimbo
03:15-3:45 Shule ya Sabato:Uongozi wa Shule ya Sabato
03:45-4:45 Mwongozo wa Kujifunza Biblia: Wote

MATANGAZO YA KANISA:
04:45-5:00 Matangazo: Mzee wa Kanisa wa Zamu
1.    Tunapenda kuwakaribisha wageni wote na waumini wa kanisa hili katika ibada takatifu Sabato ya leo.
2.    Leo ni siku maalum ya Rally ya Uchapaji, hivyo tutachangia ununuzi wa vitabu.
3.    Leo mchana tutakuwa na somo la mchana kuanzia saa 9 alasiri, wote tuhudhurie.
4.    Kesho tarehe 29/4/2012 lutakuwa na safari ya watoto kwenda Bagamoyo, gharama ni Tshs. 7000/= kwa mkubwa na Tshs. 5500/= kwa mtoto hiyo ni chakula pamoja na usafiri wa kwenda na kurudi.
5.    Vijana wote  wabakie nyuma mara baada ya ibada kuna jambo la muhimu.
6.    Zoezi la upigaji picha kwa waumini wa kanisa ili kuweka kumbukumbu katika utaratibu mzuri linaendelea, hakikisha umefikiwa na wahusika.
7.    Tunahimiza waumini kuanza kutoa sadaka ya gharama ya makambi kuanzia sasa goli la kanisa letu ni Tshs. 2,021,965/= na pia sadaka ya gharama ya efoti ambayo ni Tshs. 5,230,200/= 
8.    Wazazi wa wanachama wa PFC & AC mnaombwa kuwanunulia watoto wenu sare zao mapema.
9.    Tunawakumbusha waumini kutoa sadaka ya rambirambi Tshs. 1,200/= kwa mwezi, tuzingatie hilo.
10.    Wazee wa Kanisa wanaendelea kutembelea waumini.
11.    Mzee wa zamu ni A. Marwa.

 IBADA KUU:
05:00-6:30 WAHUDUMU IBADA KUU
    Mwenyekiti: Damas Mahimbali
     Fungu kuu: Philip Muhochi
    Mhubiri: Ladyanna Maganda
    Somo la Sadaka: Charles Mbwana

KWA WATOTO:-
    Msafiri John



ANGALIZO: “Uamsho na Matengenezo”

Ellen G. White ana haya ya kusema kuhusiana na hatari inayowakabili watoto na vijana wetu....

“Katika wakati huu wa hatari kubwa kwa vijana, majaribu yanawazunguka kila upande; wakati ambapo ni rahisi kwa watoto na vijana kuchukuliwa na mawimbi ya majaribu, nguvu kubwa sana inahitajika ili kukabiliana na mawimbi hayo. Kila shule ya Kiadventista inapaswa kuwa mji wa kimbilio kwa watoto na vijana walio majaribuni, mahali ambapo matatizo yao yanapaswa kushughulikiwa kwa subira na busara”. (Education, uk. 293)

No comments:

Post a Comment