UTARATIBU WA IBADA: 15/10/2011
1.0 SHULE YA SABATO:
2:00-3:00 Darasa la Waalimu: Uongozi wa Shule ya Sabato
3:00-3:15 Tumsifu BWANA: Kiongozi wa Nyimbo
3:15-3:45 Shule ya Sabato: Shule ya Sabato
3:45-4:45 Mwongozo wa Kujifunza Biblia: Wote
2.0 MATANGAZO YA KANISA:
v 4:45-5:00 Matangazo: Mzee wa Kanisa wa zamu
2.1 Tunapenda kuwakaribisha wageni wote na waumini wa kanisa hili katika
ibada takatifu Sabato ya leo.
2.2 Leo mchana kutakuwa na semina ya waalimu wa shule ya sabato, tafadhali wote tuhudhurie bila kukosa.
2.3 Sabato ya tarehe 19/11/2011 ni sabato maalum ya Kaya na Familia, wote tujiandae kushiriki.
2.4 Waumini wote mnakumbushwa kujiandaa kuchanga kwa ajili ya ujenzi wa kanisa letu kwenye siku ya majengo itakayofanyika tarehe 5/11/2011
2.5 Wakuu wote wa idara pamoja na kamati zenu mnakumbushwa kuleta mipango pamoja na bajeti zenu za mwaka ujao mapema mwisho ni mwezi huu.
2.6 Baraza la idara ya Vijana litakaa leo saa 10 jioni wajumbe wote muhudhurie.
2.7 Kamati ya idara ya watoto itakuwa na kikao chake leo mchana.
2.8 Kila familia na kaya inakumbushwa kufanya maombi kila saa moja asubuhi na saa moja jioni, ikiwa ni mpango wa kanisa letu ulimwenguni kote.
2.9 Tunatangaza ndoa kwa mara ya tatu kati ya Nassoro Waziri na Jane Ringia Kimaro wote ni washiriki wetu itakayofungwa hapa Kanisani tarehe 16/10/2011.
2.10 Waumini wote mnaombwa kuzingatia ratiba ya kanisa, hasa vipindi vya mchana na siyo kukaa kwenye vikundi vikundi wakati kunavipindi vya kanisa vinaendelea. Tafadhali sana tuzingatie hilo.
2.11 Mzee wa zamu wiki ijayo ni Leonard Mahinyira, kanisa la Watoto ni Msafiri John.
3.0 IBADA KUU:
v 5:00-6:30 WAHUDUMU IBADA KUU:
Mwenyekiti: Yared Omolo
Fungu Kuu: Eliamani Safiel
Hubiri: Daniel Sempambo
Sadaka: Elishama Marwa
ANGALIZO: Uamsho na Matengenezo ni mpango wa kanisa ulimwenguni kote:
ü Kanisa linajiandaa kupaa hivyo kumbuka kuomba kila saa 1 asubuhi na saa 1 jioni kwa ajili ya kupokea Roho Mtakatifu atakaye kuwezesha kumtumikia MUNGU
ANDAA SADAKA YAKO KWA AJILI YA UJENZI WA KANISA MAPEMA. Sabato ya kuchangia ujenzi ni tarehe 5/11/2011.
No comments:
Post a Comment