Friday, October 28, 2011

UTARATIBU WA IBADA: 29/10/2011

1.0 SHULE YA SABATO:
         2:00-3:00 Darasa la Waalimu: Uongozi wa Shule ya Sabato
 3:00-3:15 Tumsifu BWANA: Kiongozi wa Nyimbo
 3:15-3:45 Shule ya Sabato: Shule ya Sabato
 3:45-4:45 Mwongozo wa Kujifunza Biblia: Wote
      
2.0 MATANGAZO YA KANISA:
v  4:45-5:00 Matangazo: Mzee wa Kanisa wa zamu
      2.1 Tunapenda kuwakaribisha wageni wote na waumini wa kanisa hili katika
       ibada takatifu Sabato ya leo.
      2.2 Leo tutachangia vijana wanaokwenda kambini huko Ifakara Kibaoni-Morogoro.
      2.3 Sabato ya tarehe 19/11/2011 ni sabato maalum ya Kaya na Familia, wote tujiandae kushiriki.
      2.4 Waumini wote mnakumbushwa kujiandaa kuchanga kwa ajili ya ujenzi wa kanisa letu kwenye siku ya majengo itakayofanyika tarehe 5/11/2011
      2.5 Wakuu wote wa idara pamoja na kamati zenu mnakumbushwa kuleta mipango pamoja na bajeti zenu za mwaka ujao mapema mwisho ni mwezi huu.
      2.6 Wanachama wote wa Amo & Dorcas mnaombwa kubakia nyuma mara baada ya ibada ili muonane na kiongozi wenu.
      2.7 Mashauri ya kanisa itafanyika tarehe 13/11/2011 saa 8 mchana, panga kufika siku hiyo.
      2.8 Kila familia na kaya inakumbushwa kufanya maombi kila saa moja asubuhi na saa moja jioni, ikiwa ni mpango wa kanisa letu ulimwenguni kote.
      2.9 Idara ya watoto itakuwa na uinjilisti mitaa (kusambaza vijuzuu) siku ya tarehe 6/11/2011
      2.10 Wale wote wanaokwenda kambi la vijana wakutane leo saa kumi jioni.
      2.11 Leo saa kumi jioni kutakuwa na kikao cha baraza la shule ya sabato wajumbe mfike.
      2.12 Mzee wa zamu wiki ijayo ni A. Marwa, kanisa la Watoto ni M. John. 




3.0 IBADA KUU:
v  5:00-6:30 WAHUDUMU IBADA KUU:
Mwenyekiti: Yohana William
Fungu Kuu: Paulo Samwel
Hubiri: Julius Okoth
Sadaka: Eliya Marwa

v  KANISA LA WATOTO
Hubiri: Mwita Stephen
ANDAA SADAKA YAKO KWA AJILI YA UJENZI WA KANISA MAPEMA. Sabato ya kuchangia ujenzi ni tarehe 5/11/2011

No comments:

Post a Comment