1.0 SHULE YA SABATO:
2:00-3:00 Darasa la Waalimu: Uongozi wa Shule ya Sabato
3:00-3:15 Tumsifu BWANA: Kiongozi wa Nyimbo
3:15-3:45 Shule ya Sabato: Shule ya Sabato
3:45-4:45 Mwongozo wa Kujifunza Biblia: Wote
2.0 MATANGAZO YA KANISA:
v 4:45-5:00 Matangazo: Mzee wa Kanisa wa zamu
2.1 Tunapenda kuwakaribisha wageni wote na waumini wa kanisa hili katika
ibada takatifu Sabato ya leo.
2.2 Leo ni siku maalum ya kuchangia ujenzi wa kanisa, toa kadri MUNGU alivyokubariki, usiogope pia kumwekea MUNGU nadhiri yako ambayo utahitimiza kabla ya mwaka kuisha. Tunahitaji kiasi cha Tshs. 7,126,000/= kwa ajili ya kufunga gypsum, kila gypsum moja ni Tshs 16,000/=
2.3 Sabato ya tarehe 19/11/2011 ni sabato maalum ya Kaya na Familia, wote tujiandae kushiriki.
2.4 Baraza la kanisa rasmi litafanyika kesho tarehe 6/11/2011 wajumbe mfike kwa wakati saa 2 asubuhi, pia wakilisheni tarifa zenu kwa Katibu mapema.
2.5 Vijana wa kanisa wameondoka kwenda kambini huko Ifakara, wameenda 6 na kesho wataenda wengine 5 na Mkuu wa msafara ni Mzee wa Kanisa Msafiri John.
2.6 Wana wa kike wote wabakie nyuma mara baada ya ibada.
2.7 Mashauri ya kanisa itafanyika tarehe 13/11/2011 saa 8 mchana, panga kufika siku hiyo.
2.8 Kila familia na kaya inakumbushwa kufanya maombi kila saa moja asubuhi na saa moja jioni, ikiwa ni mpango wa kanisa letu ulimwenguni kote.
2.9 Kesho Idara ya watoto itakuwa na uinjilisti mitaa (kusambaza vijuzuu) wazazi mnakumbushwa kuwapatia watoto nauli na kuhakikisha wanawahi kufika kesho asubuhi.
2.10 Wale wote wanaokwenda kambi la vijana wakutane leo saa kumi jioni.
2.11 Kamati ya watoto itakuwa na kikao chake leo mchana, wajumbe wafike bila kukosa.
2.12 Mzee wa zamu wiki ijayo ni L. Mahinyira, kanisa la Watoto ni T. Mbonea.
3.0 IBADA KUU:
v 5:00-6:30 WAHUDUMU IBADA KUU:
Fungu Kuu:
Hubiri: IDARA YA MAJENGO
Sadaka:
v KANISA LA WATOTO:
Hubiri: Miriam Chilagi
No comments:
Post a Comment