Friday, December 30, 2011

UTARATIBU WA IBADA  31/12/2011

1.0 SHULE YA SABATO:
         2:00-3:00 Darasa la Waalimu: Uongozi wa Shule ya Sabato
 3:00-3:15 Tumsifu BWANA: Kiongozi wa Nyimbo
 3:15-3:45 Shule ya Sabato: Uongozi wa Shule ya Sabato
 3:45-4:45 Mwongozo wa Kujifunza Biblia: Wote
      
2.0 MATANGAZO YA KANISA:
v  4:45-5:00 Matangazo: Mzee wa Kanisa wa zamu
      2.1 Tunapenda kuwakaribisha wageni wote na waumini wa kanisa hili katika
       ibada takatifu Sabato ya leo.
      2.2  Leo ni meza ya BWANA, wote mnakaribishwa kushiriki baada ya huduma hiyo tutakula chakula cha mchana pamoja na kuendelea na vipindi vya mchana. Tafadhali usiache kushiriki katika huduma hizo.
      2.3 Sabato ya tarehe 7/1/2012 tutasali mtaa mzima wa Ilala ili kumuaga Mchungaji Mlwambo anayehamia Mtaa wa Misufini, Morogoro.
      2.4 Tarehe 8/1/2012 tutakuwa na mashauri ya kanisa saa 8 mchana, panga kuhudhuria.
      2.5 Kila familia na kaya inakumbushwa kufanya maombi kila saa siku saa 1 asubuhi na jioni sambamba na hilo mchungaji na wazee wanaendelea kutembelea waumini majumbani.
      2.6 Tunahimizwa kuendelea kuwaombea na kuwapatia faraja ya kimwili na kiroho wenzetu waliopatwa na janga la mafuriko. Tunawashukuru wale waliotoa fedha na mali kusaidia na hata wale waliowapatia hifadhi. MUNGU awabariki huo ndio ukristo.
      2.7 Baraza la mtaa litakuwa na kikao leo mchana saa 11:00 jioni, wajumbe mzingatie.
      2.8 Wakuu wa Idara andaeni tarifa zenu za mwaka na mzikabidhi kwa Katibu wa Kanisa mapema.
     2.9 Tunatangaza nafasi ya kazi ya ulinzi wa kanisa, wanaohitaji walete maombi kwa Katibu wa kanisa.
     2.10 Mzee wa zamu ni T. mbonea, Watoto M. John

3.0 IBADA KUU:
v  5:00-6:30 WAHUDUMU IBADA KUU:
v  IBADA KUU:
Fungu Kuu:        Paschal Gomba
Somo la sadaka: Ezekiel Fungo
Mwenyekiti:        Chediel mbwambo
                            Hubiri:                Pr. Eldad Mlwambo


v  KWA WATOTO;
·         Mhubiri: Grace Edward

RATIBA YA MCHANA
MUDA
TUKIO
MUHUSIKA
08:00-09:00
Nyimbo
Joseph majura
09:00-09:20
Wanafunzi bora wa Shule ya Sabato
Yared Omollo
09:20-10:00
Somo Maalum
Pr. Eldad Mlwambo
10:00-11:00
Zawadi/Pongezi kwa watendakazi bora 2011
Maurice Rondo
 
ANGALIZO: Mwaka umeisha, tafakari ulivyomtumikia MUNGU kwa mwaka 2011 na ujipange kumtumikia kwa nguvu, akili na uwezo zaidi katika mwaka wa 2012.

No comments:

Post a Comment