MATANGAZO YA KANISA:
1. Tunapenda kuwakaribisha wageni wote na waumini wa kanisa hili katika ibada takatifu Sabato ya leo.
2. Leo tunahitimisha juma la maombi la Vijana.
3. Leo alasiri tutakuwa na muhandara wa AMR wote tuhudhurie.
4. Wakuu wa Idara ya huduma za Watoto na Wanawake watakuwa na mkutano wao kuanzia tarehe 28/3-1/4/2012 huko Bagamoyo.
5. Tarehe 25-26/3/2012 kutakuwa na mafunzo ya cheti kwa Wazee wa Kanisa yatakayofanyika huko Kanisani Mwenge kuanzia asubuhi hadi jioni, wahusika jiandaeni.
6. Sabato ya tarehe 31/3/2012 itakuwa ni meza ya BWANA tujiandae kushiriki.
7. Kumbuka j5 wiki ijayo ni siku ya kufunga kwa kanisa zima, kuombea hali ya kiroho ya kanisa, maendeleo ya kanisa na mahitaji ya kila mmoja wetu.
8. Rally ya Idara ya uchapaji duniani itafanyika tarehe 21/4/2012, jiandae kuchangia ununuzi wa vitabu kwa ajili ya kuokoa ulimwengu.
9. Zoezi la upigaji picha kwa waumini wa kanisa ili kuweka kumbukumbu katika utaratibu mzuri linaendelea, hakikisha umefikiwa na wahusika na wale waliopiga picha sabato iliyopita wanaombwa kurudia tena maana kuna tatizo la kiufundi lilitokea.
10. Tunahimiza waumini kuanza kutoa sadaka ya gharama ya makambi kuanzia sasa goli la kanisa letu ni Tshs. 2,021,965/= na pia sadaka ya gharama ya efoti ambayo ni Tshs. 5,230,200/=
11. Mzee wa zamu ni L. Mahinyira, Watoto ni M. John
IBADA KUU:
05:00-6:30 WAHUDUMU IBADA KUU
Mwenyekiti: Eliamani Sengesa
Fungu kuu: Charles Gibson
Mhubiri: Yohana William
Somo la Sadaka: Ayoub Charles
Fungu Kuu:- Ufunuo 3:1
No comments:
Post a Comment