TMI NI NINI?
TMI ni kifupisho cha maneno matatu (3) ya lugha ya kiingereza ambayo ni "Total Member Involvement". Maneno haya yana maana ya "Kuhusishwa kikamilifu kwa kila muumini".
Kaulimbiu hii inatumika sasa katika Kanisa la Waadventista Wa Sabato ulimwenguni kote ikilenga kuhimiza waumini ulimwenguni kote kujitoa kikamilifu katika kutumika shambani mwa BWANA yaani kupeleka injili.
TMI ni mpango wa Kanisa ulimwenguni kote ambao unahusisha kila muumini, kila kanisa, kila hatua ya uongozi, kila huduma inayogusa jamii, taasisi na mtu mmoja mmoja.
Kristo alisema "Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; Na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari" Mathayo 28: 19,20
KARIBU UJIUNGE NA MPANGO HUU AMBAO KRISTO MWENYEWE ALIUANZISHA.

No comments:
Post a Comment