Friday, September 1, 2017

SABATO





SABATO

Nalifurahi waliponiambia, Na twende nyumbani kwa Bwana” Zaburi 122:1

Mungu ametupatia siku zote sita za kutenda mambo yetu, na kuitenga siku moja tu kwa ajli yake. Hii yapaswa kuwa siku ya baraka kwetu, siku ambayo tunaweka mambo yetu kando na kuelekeza mawazo yetu kwa Mungu na mbingu. Katika siku hii mioyo yetu inapaswa kuamshwa kwani tunakutana na Mungu na Kristo mwokozi wetu. Tunaweza kumwona kwa imani. Yeye anasubiri kurejeza na kubariki kila roho.


Sabato ni wasaa wa Mungu. Aliibariki na kuitakasa siku ya saba. Aliiweka maalum kwa ajili ya mwanadamu kuitunza kama siku ya ibada


Tunapaswa kufurahi na kukuza roho ya ibada ya kweli, roho ya kujiweka wakfu katika siku takatifu ya Bwana. Tunapaswa kukusanyika pamoja tukiamini kuwa tutapokea faraja na tumaini, nuru na Amani toka kwa Kristo Yesu.

2 comments: